Search a title or topic

Over 20 million podcasts, powered by 

Player FM logo

Rfi Kiswahili Podcasts

show episodes
 
Artwork

1
Habari RFI-Ki

RFI Kiswahili

icon
Unsubscribe
icon
icon
Unsubscribe
icon
Weekly+
 
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
  continue reading
 
Artwork

1
Jukwaa la Michezo

RFI Kiswahili

icon
Unsubscribe
icon
icon
Unsubscribe
icon
Monthly+
 
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.
  continue reading
 
Artwork

1
Wimbi la Siasa

RFI Kiswahili

icon
Unsubscribe
icon
icon
Unsubscribe
icon
Monthly+
 
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
  continue reading
 
Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.
  continue reading
 
Artwork

1
Siha Njema

RFI Kiswahili

icon
Unsubscribe
icon
icon
Unsubscribe
icon
Weekly
 
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
  continue reading
 
Artwork

1
Jua Haki Zako

RFI Kiswahili

icon
Unsubscribe
icon
icon
Unsubscribe
icon
Weekly
 
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.
  continue reading
 
Artwork

1
Gurudumu la Uchumi

RFI Kiswahili

icon
Unsubscribe
icon
icon
Unsubscribe
icon
Monthly+
 
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .
  continue reading
 
Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.
  continue reading
 
Artwork

1
Nyumba ya Sanaa

RFI Kiswahili

icon
Unsubscribe
icon
icon
Unsubscribe
icon
Monthly+
 
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.
  continue reading
 
Artwork

1
Mjadala wa Wiki

RFI Kiswahili

icon
Unsubscribe
icon
icon
Unsubscribe
icon
Monthly
 
Huu ni wasaa wa kukutana na wageni mbalimbali watakaokuwa wakifika katika studio zetu na kuzungumza moja kwa moja yaani LIVE. Ni mjadala wa kila Jumatano asubuhi ambao utagusa masuala muhimu yanayoibuka ndani na nje ya Bara la Afrika katika nyanja tofaut itofauti. Mjadala wa wiki ni wasaa utakaokuzungusha dunia nzima kupitia mawimbi ya RFI Kiswahili.
  continue reading
 
Artwork

1
Talisman Brisé

RFI Kiswahili

icon
Unsubscribe
icon
icon
Unsubscribe
icon
Monthly
 
Talisman Brisé ni tamthilia ya redio inayosimulia hadithi ya mtunza bustani Kwame ambaye bosi wake Profesa Omar anatekwa nyara na watu wasiojulikana. Kwa nini Profesa Omar anatekwa nyara na watu hao? Mfanyakazi wake Kwame atafanikiwa kumuokoa Bosi wake? Fuatilia haya kwenye tamthilia ya Talisman Brise hapa rfi kila siku ya jumapili ndani ya Makala ya Changu Chako Chako Changu.
  continue reading
 
Artwork

1
Muziki Ijumaa

RFI Kiswahili

icon
Unsubscribe
icon
icon
Unsubscribe
icon
Monthly
 
Makala ambayo inakupa nafasi ya kujua masuala mbalimbali ya Muziki na Burudani. Ndani ya makala haya utapata taarifa za wanamuziki, historia zao na bila kusahau mahojiano na wanamuziki mbalimbali. Hii ni fursa ya pekee kwa wasikilizaji kujiliwaza baada ya kazi za juma zima kupitia burudani ya muziki. Makala ya muziki ijumaa pia itakuwezesha kufahamu wasanii kutoka sehemu mbalimbali duniani na kujua wanafanya nini.
  continue reading
 
Loading …
show series
 
Viongozi wa dunia, wataalam wa Afya na wanasayansi wanakutana Afrika Kusini siku chache kabla kikao cha G20, ili kuanganzia kuhusu njia za kufadhili afya bila kutegemea ufadhili wa kigeni.Tumemuuliza msikilizaji maoni yake kuhusu uwezo wa mataifa ya Afrika kufadhili miradi ya afya?By RFI Kiswahili
  continue reading
 
Miongoni mwa matukio makubwa yaliyojiri wiki hii ni pamoja na wakenya kuomboleza kifo cha mwanasiasa mashuhuri aliyewahi kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Raila Amolo Odinga, kuzinduliwa kwa jukwaa jipya la kisiasa : Okoa DR Congo, kuendelea kwa kampeni za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu kule Tanzania, kuapishwa kwa kiongozi wa kijeshi wa Madagascar, na…
  continue reading
 
Kuanzia yale ya nazi hadi mizeituni, mboga hadi kanola, parachichi hadi mafuta ya wanyama maswali yameibuka kuhusu tunajuaje yapi mazuri ya kutumia, na ikiwa tunapaswa kuepuka yoyote yale kabisa Watalaam wa afya wanahoji mafuta ni kiungo muhimu katika mwili wa binadaam kwa kuwa huchangia madini muhimu na pia husaidia utendakazi wa viungo muhimu mwi…
  continue reading
 
Hivi leo viongozi wa dunia akiwemo rais wa Marekani, Donald Trump, wanakutana Misri kujadili mustakabali wa eneo la Gaza, baada ya makubaliano ya kihistoria ya wiki iliyopita. Makubaliano haya yameshuhudia kuachiwa kwa mateka, wafungwa na kusitishwa kwa vita vya Gaza. Tunakuuliza, unaamini makubaliano kati ya Hamas na Israel safari hii yatadumu?Nin…
  continue reading
 
Karibu katika makala ya leo Jumapili Changu Chako Chako Changu ambapo leo nakuletea sehemu ya pili ya siku ya kimataifa ya ukalimani na tafsiri, na kwenye le parler francophone nitakujuwa kinachoendelea kwenye vituo vya Alliance Francaise za Ukanda na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Mace Ice. Mimi ni Ali Bilali mtangazaji wako asiependa makuu…
  continue reading
 
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na tathmini ya timu za Afrika ambazo zimefuzu Kombe la Dunia 2026 na ni nani ambao wana nafasi ya kufuzu kuelekea raundi ya mwisho ya mechi za kufuzu, FIFA yateua wajumbe kutoka CECAFA, Herita Ilunga ndiye mkurugenzi mpya wa FECOFA nchini DRC, kocha wa zamani wa Yanga Nassredine Nabi waachana na Kaizer Chiefs, nyota ta…
  continue reading
 
Habari kuu wiki hii ni pamoja Israel kuanza kuwaondoa wanajeshi wake kwenye baadhi ya maeneo ya Gaza, rais wa Ufaransa amteua tena Sebastien Lecornu kuwa waziri mkuu huku kukiwa na mvutano wa kisiasa, rais wa DRC, Félix Tshisekedi, amtaka mwenzake wa Rwanda, Paul Kagame, kuwaamuru waasi wa M23 kuacha vita mashariki mwa Congo, siasa za kikanda, yali…
  continue reading
 
Msikilizaji kesho Ijumaa oktoba 10 kamati inayotoa tuzo za kimataifa za Nobel itamtangaza mshindi, wakati huu watu wengi wakiwa wamempendekeza rais wa Marekani Donald Trump kutokana na mchango wake wa kutafuta amani mashariki ya kati, hata hivyo wadadisi wanasema kiongozi huyo hawezi kupewa tuzo hiyo. Unafikiri ni Kiongozi gani anastahili kupewa tu…
  continue reading
 
Habari rafiki ya jumatano octoba 08 imeangazia vitendo vya utekaji nyara ambavyo vimeongezeka katika nchi za ukanda wa Afrika mashariki, hivi karibuni nchini Uganda wanaharakati wawili kutoka nchini Kenya walikamatwa baada ya kuhudhuria mkutano wa kisiasa wakati nchini Tanzania, aliyekuwa balozi wa nchi hiyo huko Cuba Humphrey Polepole alitekwa na …
  continue reading
 
Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa waasi wa AFC/M 23 wanaendelea kujiimarisha zaidi kisiasa na kiuchumi, katika maeneo wanayodhibiti, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, licha ya kuwepo kwa mkataba wa Washington uliokubaliwa kati ya DRC na Rwanda kuhusu namna ya kupata mwafaka wa kudumu. Hatua hii inamaanisha nini ? Tunachambua.…
  continue reading
 
Karibu katika Makala yetu ya leo Jumapili changu chako chako changu Makala ambayo khukuletra historia ya mambo mbalimbali utamaduni le parler francophone na Muziki, na eo nakuletea maadhimisho ya siku ya kimataifa ya ukalimani na utafsiri ambayo huamdihimishwa kila septemba 30 ya kila mwaka. Kwenye le parler francophone nitakujuwa yaliojiri kwenye …
  continue reading
 
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na Rwanda kuwa taifa la kwanza Afrika kudhamini vilabu vya basketboli Ulaya, nini kinachoendelea klabuni Simba washikadau wanaendelea kuondoka, TP Mazembe yajiondoa katika Chama cha Vilabu vya Soka vya Kongo, Afrika inaandaa kwa mara ya kwanza mashindano ya boti za umeme nchini Nigeria, mwanawe Zidane aitwa kikosini Al…
  continue reading
 
Kumekuwa na hisia mseto kuhusu hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya rais mstaafu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila, uzinduzi wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwakani nchini Uganda, hali ya nchini Tanzania wakati huu wananchi wakijiandaa kushiriki uchaguzi wa oktoba 29 mwaka huu, maandamano ya vijana Gen Z nchini Madagascar, na m…
  continue reading
 
Kama kuna kipindi watu wengi huwa tumbo joto, ni kusubiri matokeo ya kipimo cha HIV au magonjwa mengi ya zinaa.Au kuambiwa huna uwezo wa kizazi. Hata hivyo unapofanya vipimo hivyo itakuokoa kufanya makosa ambayo yanaweza kuathiri familia yako baadaye. Ikiwa utapima baadhi ya vipimo hivi muhimu utaweza kujipanga kifedha na kuchagua matibabu ambayo y…
  continue reading
 
Mahakama ya kijeshi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC imemhukumu rais mstaafu wa nchi hiyo Joseph Kabila Kabange adhabu ya kifo bila ya yeye mwenyewe kuwepo mahakamani, ikimtia hatiani kwa usaliti na uhalifu dhidi ya binadamu. Chama chake PPRD kimesema kesi hiyo ni ya kisiasa dhidi ya mpinzani mkubwa wa serikali. Mwandishi wetu Ruben Luku…
  continue reading
 
Kampeni za uchaguzi mkuu nchini Uganda, uliopangwa kufanyika Januari 12, 2026, zilianza Septemba 29. Kuna wagombea wanane wa urais, akiwemo kiongozi wa muda mrefu Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 81, ambaye ameongoza nchi hiyo kwa miaka 39. Mpinzani wake mkuu ni Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, mwenye umri wa miaka 43. Nini kinachotara…
  continue reading
 
Mkataba wa kibiashara kati ya Afrika na Marekani maarufu kama AGOA umefika tamati, ni mkataba uliokuwa unatoa fursa kwa nchi za Afrika kufikia soko la Marekani bila vikwazo vya kiushuru, bara hili likitengeneza faida ya mabilioni ya dola kupitia mkataba huu, hata hivyo kukoma kwake tayari kunashuhudiwa athari yalke kwenye baadhi ya nchi, kuanzia ka…
  continue reading
 
Loading …
Copyright 2025 | Privacy Policy | Terms of Service | | Copyright
Listen to this show while you explore
Play